Thursday, May 31, 2012

ABIDAL ANAWEZA KUREJEA UWANJANI - DAKTARI.

DAKTARI aliyemfanyia upasuaji beki wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Barcelona, Eric Abidal amesema kuwa mchezaji huyo anaweza kurejea tena uwanjani baada ya kufanyiwa upasuaji wa kupandikiza ini. Abidal mwenye umri wa miaka 32 alifanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe uliokuwa umeota katika ini lake mwaka uliopita lakini baada ya kurejea tena uwanjani tena alilazimika kufanyiwa upasuaji mwingine wa kupandikiza sehemu ya ini lingine ambalo mpwa wake alijitolea April 10 mwaka huu. Daktari huyo aitwae Juan Carlos Garcia-Valdecasas amesema kuwa ni juu ya mchezaji mwenyewe kuamua kuendelea kucheza au kupumzika kabisa yeye hawezi kumzuia, kwani akiendelea vizuri kama hivi sasa haoni sababu ya mchezaji huyo kushindwa kucheza. Valdecasas aliendelea kusema kuwa ini ni kiungo ambacho huwa kinakuwa katika kipindi cha miezi mitatu hivyo Abidal atakuwa akipona taratibu katika kipindi cha miezi sita au mwaka mmoja na baada ya hapo anaweza kuendelea na maisha yake ya kawaida. Wachezaji wa Barcelona walivaa jezi anayotumia mchezaji huyo wakati wakisheherekea ushindi wa Kombe la Mfalme waliloshinda baada ya kuifunga Athletico Bilbao Ijumaa iliyopita.

No comments:

Post a Comment