Wednesday, May 30, 2012

BARCELONA KUFANYA ZIARA MOROCCO.

KLABU ya Barcelona inatarajiwa kufanya ziara ya kimichezo nchini Morocco Julai 28 mwaka huu ambapo wakiwa nchini humo watacheza mchezo wa kirafiki na moja vilabu vya nchi hiyo jijini Tanger. Wizara ya michezo nchini humo ilithibitisha ziara hiyo ambapo wanatarajia kuwalipa kiasi cha euro milioni moja Barcelona ambao ni mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya 2011. Ofisa Habari wa wizara hiyo Hamid Faridi amesema kuwa mji wa Tangier ambao uko Kaskanini mwa nchi hiyo ndio utakuwa mwenyeji wa timu hiyo ambayo itakwenda huko na nyota wao wote akiwemo Lionel Messi. Mchezo huo wa kirafiki umeandaliwa na kamati iliyoteuliwa na wizara ya michezo ya nchi hiyo pamoja na shirika la kitaifa la utekelezaji na usimamizi wa viwanja.

No comments:

Post a Comment