Tuesday, May 29, 2012

HAZARD KUJIUNGA NA CHELSEA.

Eden Hazard.
KIUNGO nyota wa kimataifa wa Ubelgiji na klabu ya Lille ya Ufaransa, Eden Hazard amesema kuwa ameamua kujiunga na mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya timu ya Chelsea badala ya Manchester City au Manchester United. Hazard ambaye ana umri wa miaka 21 aliandika katika mtandao wake wa kijamii wa twitter kuwa anatarajia kusaini katika klabu ya Chelsea na kukomesha uvumi ambao ulikuwa umesambaa kuwa atajiunga na aidha United au City katika kipindi hiki cha usajili. Mchezaji huyo amenyakuwa tuzo za mchezaji bora wa Ligi Kuu nchini Ufaransa maarufu kama Ligue 1amekiongoza kikosi cha Lille kunyakuwa taji la ligi hiyo mwaka 2011 na kufunga mabao 20 msimu ambayo yameiwezesha klabu hiyo kushika nafasi ya tatu msimu huu hivyo kukata tiketi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao. Hazard alitua Lille akiwa na umri wa miaka 16 ambapo haraka haraka alipanda kiwango na kujikuta akiwa katika kikosi cha kwanza cha Lille na alitangaza msimu wa mwisho kuwepo katika klabu hiyo Octoba mwaka jana.

No comments:

Post a Comment