POLISI mmoja wa Dubai anakabiliwa na kifungo cha miezi sita jela na faini ya euro 124,000 kwa kutuma picha za video za pasi ya kusafiria ya mshambuliaji nyota wa Barcelona Lionel Messi, katika mitandao ya kijamii. Polisi huyo wa Uwanja wa Ndege aliyejulikana kwa jina la J.J anatuhumiwa na waendesha mashitaka kwa kuingilia mfumo wa mawasiliano na alikiri kosa la kuvunja Sheria ya Mtandao lakini aliomba kusamehewa. Messi alitua Dubai mwishoni mwa Desemba kuhudhuria sherehe za tuzo ya Globe Soccer ambao alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka na polisi huyo aliomba kama anaweza kupiga picha na nyota huyo lakini ilishindikana kwasababu alikuwa amechoka. Polisi huyo mwenye umri wa miaka 26, baadae aliingia katika chumba cha mawasiliano na kuirekodi video wakati Messi akionyesha pasi yake ya kusafiria kwa wana usalama kabla ya kuituma katika mtandao wa Snapchat.
No comments:
Post a Comment