Wednesday, January 20, 2016

TETESI ZA USAJILI ZILIZOJIRI HUKO MAJUU.

MENEJA wa Manchester United, Louis van Gaal yuko tayari kuondoka katika timu hiyo majira ya kiangazi ikiwa ni mwa mmoja kabla ya kumalizika kwa mkataba wake wa miaka mitatu, sababu kubwa ikiwa ni shinikizo na shutuma anazopambana nazo.
Chanzo: Daily Mirror

KLABU ya West Ham United, inajipanga kumuwania mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge. West Ham imefikia hatua hiyo kufuatia meneja wa Liverpool Jurgen Klopp kutishwa na majeruhi ya Sturridge hivyo kuwa tayari kupokea kitita cha paundi milioni 18.
Chanzo: Brentwood Gazette

MENEJA wa Watford Quique Sanchez Flores ameamua kuacha kumuwania Emmanuel Adebayor na kuifanya Crystal Palace kuwa na nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliaji huyo ambaye yuko huru kwasasa baada ya kuachwa na Tottenham Hotspurs.
Chanzo: Evening Standard

MENEJA wa Liverpool Jurgen Klopp ameripotiwa kusisitiza kusajiliwa kwa marc-Andre Ter Stegen ili kuleta ushindani kwa Simon Mignolet ambapo klabu hiyo inedaiwa kutoa ofa ya paundi milioni 10.8 lakini Barcelona wao wanataka paundi milioni 23 kwa kipa huyo.
Chanzo: Don Balon

KLABU ya Tottenham Hotspurs inajiandaa kumuwania kiungo wa Coventry James Maddison na kama wakifanikiwa watamuacha kwa mkopo katika klabu hiyo ya daraja la kwanza mpaka mwishoni mwa msimu huu.
Chanzo: The Independent

KLABU ya Liverpool ilikaribia kumsajili Dele Alli kutoka timu ya MK Dons kiangazi mwaka jana lakini walichemka kwa kumpa ofa ya mshahara wa paundi 4,000 kwa wiki nyota huyo ambaye kwasasa anang’aa katika klabu ya Tottenham Hotspurs.
Chanzo: Daily Mail

WAKALA wa Ezequiel Lavezzi, Alessandro Moggi ametua jijini London leo kufanya mazungumzo na Chelsea, lakini haijajulikana kama wanazungumza kuhusu uhamisho wa mshambuliaji kwenda PSG kipindi hiki cha Januari au kiangazi.
Chanzo: Sky Sport Italia

KLABU ya Chelsea inadaiwa kutaka kusajili wachezaji watatu ambao ni Alexandre Pato, Aymen Abdennour na Alex Teixeira kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili majira ya kiangazi huku wakiwaruhusu Papy Djilobodji na Charly Musonda kuondoka kwa mkopo.
Chanzo: Daily Mail

KLABU ya Liverpool inaripotiwa kuwepo katika mazungumzo na Juventus kwa ajili ya kumsajili Alvaro Morata kwa kitita cha euro milioni 58.1, wakati Arsenal na Manchester United nazo pia zikimmezea mate nyota huyo.
Chanzo: Gazzetta dello Sport

No comments:

Post a Comment