Friday, January 29, 2016

VIDIC AAMUA KUTUNDIKA DARUGA ZAKE.

NAHODHA wa zamani Manchester United, Nemanja Vidic ametangaza kustaafu rasmi soka baada ya kuachwa na klabu ya Inter Milan. Beki huyo wa kati raia wa Serbia, ambaye alianza soka lake katika klabu ya Red Stars Belgrade kabla ya kutua Old Trafford ambako alidumu kwa miaka nane na kufanikiwa kunyakuwa mataji matatu ya Ligi Kuu, matatu ya Kombe la Ligi na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa chini ya Sir Alex Ferguson. Vidic alitimkia Inter mwaka 2014 ambako alifanikiwa kucheza mechi 28, hata hivyo toka msimu huu umeanza hajafanikiwa kucheza kutokana na matatizo ya ngiri na maumivu ya mgongo yaliyomsumbua. Katika taarifa yake, Vidic amesema anadhani wakati wake wa kutundika daruga zake umefika kwani majeruhi yanaonekana kukwamisha ndoto zake za kuendelea kucheza. Vidic aliwashukuru wachezaji, viongozi, makocha na wafanyakazi wote ambao wamekuwa pamoja naye katika kipindi chote na klabu zote alizopitia.

No comments:

Post a Comment