Friday, January 29, 2016

TETESI ZA USAJILI ZILIZOJIRI HUKO MAJUU.

KLABU ya Chelsea inaripotiwa kumpa kipaumbele katika mipango yao kocha wa timu ya taifa ya Italia Antonio Conte, wakati wakitafuta mbadala wa muda mrefu wa Jose Mourinho wakati meneja wa muda wa Guus Hiddink atakapomaliza muda wake.
Chanzo: Daily Maily

KLABU ya Newcastle United imeanza mazungumzo ya kutaka kumsajili kwa mkopo beki wa kuhsoto wa Valencia Lucas Orban.
Chanzo: Daily Mail

KLABU ya Leicester City inaripotiwa kukataa ofa ya euro milioni 40 kutoka Chelsea kwa ajili ya kumuachia Jamie Vardy. Ofa hiyo kutoka Chelsea inaripotiwa kumjumuisha Loic Remy.
Chanzo: Fichajes.net

KLABU ya AC Milan imekataa ofa ya Leicester City ya paundi milioni 12.2 kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa M’Baye Niang.
Chanzo: Sky Sport Italia

KLABU ya West Ham United inaripotiwa kuwa tayari kutumia fedha nyingi katika usajili wa kiangazi wakati wakijiandaa kuhamia katika uwanja wao mpya mwenye uwezo wa kubeba mashabiki 60,000 ambapo nyota wa Southampton Sadio Mane akitajwa kuwepo katika orodha ya wachezaji watakaowahitaji.
Chanzo: Brentwood Gazette

KLABU ya Liverpool imeamua kumuweka Javier Hernandez katika mipango yake wakati wakijaribu kuimarisha safu yao ya ushambuliaji ambapo inadaiwa kuwa wanaweza kulipa mpaka paundi milioni 20 kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Bayer Leverkusen.
Chanzo: The Times

KLABU ya Manchester United imeingia katika vita na Leicester City ya kumsajili mshambuliaji wa CSKA Moscow Ahmed Musa ambaye anaweza kuwagharimu kitita cha paundi milioni 19.
Chanzo: Daily Express

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger anaripotiw akutaka kuimarisha safu yake ya ushambuliaji majira ya kiangazi na moja ya wachezaji anaowahitaji ni mshambuliaji wa Hull City Abel Hernandez.
Chanzo: Tuttomercatoweb.com

KLABU ya Chelsea inadaiwa kupania kuimarisha safu yake ya ulinzi katika kipindi hiki cha usajili na tayari wameanza kumfukuzia beki wa kati wa Atletico Madrid Jose Gimenez baada ya kushindwa kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay majira ya kiangazi mwaka jana.
Chanzo: Evening Standard

No comments:

Post a Comment