Wednesday, January 27, 2016

PALACE WAMCHUKUA ADEBAYOR.

HATIMAYE klabu ya Crystal Palace imemsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Togo Emmanuel Adebayor kwa uhamisho huru mpaka mwishoni mwa msimu huu. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31, alikuwa yuko huru baada ya kuachwa na Tottenham Hotspurs Septemba mwaka jana, akiwa amefunga mabao 94 katika Ligi Kuu akiwa na Spurs, Arsenal na Manchester City. Wiki mbili zilizopita meneja wa Palace Alan Pardew alithibitisha nia yake ya kumuwania mshambuliaji huyo. Mara ya mwisho kuichezea Spurs ilikuwa ni Mei 3 mwaka jana, ambapo alicheza kwa dakika sita wakati Spurs walipochapwa bao 1-0 na City. Palace kwasasa wanashikilia nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi baada ya kucheza mechi 23.

No comments:

Post a Comment