Wednesday, January 27, 2016

GERVINHO ATIMKIA CHINA.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya AS Roma, Gervinho amehamia katika Ligi Kuu ya China akijiunga na klabu ya Hebei China Fortune FC. Nyota huyo ambaye mara mbili amewahi kuteuliwa kuwa mchezaji bora wa Ivory Coast alitoka Arsenal kwenda Roma mwaka 2013 baada ya kucheza kwa misimu miwili Uingereza. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 amefunga mabao 17 katika mechi 71 za Serie A alizoichezea Roma yakiwemo mabao sita katika mechi 14 msimu huu. Roma tayari ameanza mazungumzo ya kumchukua Stephan El Shaarawy ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Monaco akitokea AC Milan ili aweze kuziba pengo la Gervinho.

No comments:

Post a Comment