Wednesday, January 27, 2016

RUMMENIGGE AWAONYA DFB KUHUSU BOATENG.



OFISA mkuu wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge amekionya Chama cha Soka cha Ujerumani-DFB kutoingilia mipango ya kurejea uwanjani ya Jerome Boaten. Boateng alipata majeruhi mabaya ya nyonga Ijumaa iliyopita katika mchezo wa Bundesliga dhidi ya Hamburg na taarifa zilizozagaa ni kuwa atakaa nje ya uwanja kwa miezi zaidi ya minne. Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Low ambaye anatarajiwa kutangaza kikosi cha nchi hiyo Mei 31 kwa ajili ya michuano ya Euro 2016, amesema ataacha milango wazi kwa kipindi kirefu kwa ajili ya beki huyo na anamatumaini ataweza kupona kwa wakati. Hata hivyo, Rummenigge akihojiwa na wanahabari aliwaonya DFB kutoingilia suala la Boateng kwani bila hivyo watapambana nao. Rummenigge amesema Boateng ni mwajiriwa wao hivyo masuala yeyote kuhusiana na afya yake klabu ndio inapaswa kuzungumza na sio vinginevyo.

No comments:

Post a Comment