Sunday, January 24, 2016

TETESI ZA USAJILI ZILIZOJIRI HUKO MAJUU.

WAKATI wakiwa katika mipango ya kuhakikisha wanabaki kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu, Leicester City wanaripotiwa kufanya mawasiliano na klabu ya Sampdoria kwa ajili ya kutaka kumsajili mshambuliaji wao Eder.
Chanzo: Sky Sport Italia

KLABU ya Tottenham Hotspurs imemzuia Kevin Wimmer kuondoka katika timu hiyo pamoja na kuwania kwa kiasi kikubwa na klabu ya Schalke ya Ujerumani.
Chanzo: Sky Sports

KLABU ya Real Madrid inajipanga kutenga kitita cha paundi milioni 75 kwa ajili ya kumuwania mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski.
Chanzo: The Sun

KLABU ya Arsenal inaripotiwa kumfuatilia kwa karibu kumnasa kipa Arrizabalaga wa Athletic Bilbao, ambaye wanataka aje kuwa mbadala wa muda mrefu wa Petr Cech.
Chanzo: Don Balon

KLABU za Malaga, Levante na Rayo Vallecano zote zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili kwa mkopo Christian Atsu, huku chipukizi huyo wa Chelsea akikaribia kusitishiwa mkopo wake katika klabu ya Bournemouth baada ya kushindwa kucheza mechi yeyote ya Ligi Kuu.
Chanzo: Sky Sport

NAHODHA wa zamani wa kimataifa wa Ivory Coast, Didier Drogba anatarajiwa kujiunga na klabu yake ya Montreal kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya kufuatia wiki kadhaa za tetesi kuwa anaweza kupewa kibarua katika benchi la ufundi la Guus Hiddink katika klabu ya Chelsea.
Chanzo: TSN

No comments:

Post a Comment