KATIBU mkuu wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA, Gianni Infantino amesema Shirikisho la Soka Duniani-FIFA linapaswa kuandaa michuano ya Kombe la Dunia katika bara badala nchi moja au mbili. Kauli hiyo ya Infatino imekuja wakati akianza kampeni zake katika kinyang’anyiro cha urais wa FIFA ambao uchaguzi wake unatarajiwa kufanyika mwezi ujao. Infatino ameahidi michuano mikubwa ya Kombe la Dunia, mageuzi kufuatia kashfa iliyolikumba shirikisho hilo na fedha zaidi kwa nchi wanachama, kama akichaguliwa kuiongoza FIFA katika uchaguzi wa Februari 26 mwaka huu. Infatino ambaye amekuwa akifanya kazi chini rais wa UEFA aliyesimamishwa Michel Platini kwa miaka saba iliyopita amesema Kombe la Dunia kuongezwa na kufikia nchi 40 badala ya 32 za hivi sasa. Mgombea huyo amesema FIFA inapaswa kuangalia uwezekano wa kutanua michuano ya Kombe la Dunia badala ya kufanyika katika nchi moja au mbili iweze kufanyika katika bara zima husika ili kutoa nafasi kwa nchi nyingi zaidi kupata heshima na kunufaika kwa kuwa wenyeji.
No comments:
Post a Comment