Wednesday, January 20, 2016

IRAQ YATANGAZA KUMUUNGA MKONO PRINCE ALI KATIKA UCHAGUZI WA FIFA.

CHAMA cha Soka cha Iraq-IFA kimetangaza kumuunga mkono Prince Ali Bin Al Hussein wa Jordan katika kinyang’anyiro cha urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA mwezi ujao. Prince Ali anatarajiwa kupambana na rais wa Shirikisho la Soka la Asia-AFC, Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa, kaimu katibu mkuu wa zamani wa FIFA, Jerome Champagne, mwanasiasa na mfanyabiashara wa Afrika Kusini Tokyo Sexwale na katibu mkuu wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA, Gianni Infantino, katika uchaguzi huo wa Februari 26. Rais wa IFA Abdul Khaliq Masood amesema katika taarifa yake iliyotumwa FIFA kuwa wameamua kura ya nchi hiyo itakwenda kwa Prince Ali kwasababu ya mchango wake mkubwa katika maendeleo y soka ya eneo hilo. Hii ni mara ya pili kwa Prince Ali kugombea nafasi hiyo bada ya kushindwa na rais anayeondoka Sepp Blatter katika uchuguzi uliofanyika Mei mwaka jana.

No comments:

Post a Comment