Wednesday, January 20, 2016

ASHLEY COLE KUTIMKIA MAREKANI.

BEKI wa zamani wa kimataifa wa Uingereza, Ashley Cole amekubali kuhamia klabu ya Los Angeles Galaxy inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani-MLS baada ya kuondoka AS Roma. Cole mwenye umri wa miaka 35, yuko huru kujiunga na mchezaji mwenzake wa zamani wa Uingereza Steven Gerrard baada ya mkataba wake na Roma kuvunjwa kwa maelewano. Beki huyo wa zamani wa klabu za Arsenal na Chelsea alijiunga na klabu hiyo ya Serie A Julai mwaka 2014 na kufanikiwa kucheza mechi 16. Akiwa ameichezea Uingereza mechi 101, Cole amefanikiwa kunyakuwa mataji matatu ya Ligi Kuu, saba ya Kombe la FA, moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya na moja la Europa League.

No comments:

Post a Comment