Monday, January 18, 2016

RONALDO AKIRI KUWA NA MAHUSIANO MAZURI NA MESSI.

MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesisitiza kuwa sasa wana mahusiano mazuri na Lionel Messi na kutania kuwa bado anasubiri malipo yake kwa kutoa huduma ya ukalimani wakati tuzo za Ballon d’ Or. Wawili hao wamekuwa mahasimu wakubwa katika tuzo hizo kwani katika kipindi cha miaka nane iliyopita ni wao ndio wamezitawala. Lakini akihojiwa mara baada ya Madrid kushinda mabao 5-1 dhidi ya Sporting Gijon, nyota huyo wa kimataifa wa Ureno amesisitiza kuwa kwasasa wana mahusiano mazuri na nyota huyo wa Barcelona. Ronaldo amesema wamekuwa karibu zaidi na wamekuwa wakifurahia uhusiano wao mzuri kulinganisha na miaka ya nyuma. Messi na Ronaldo walipanda jukwaani pamoja ambamba na Neymar katika sherehe za tuzo ya Ballon d’Or jijini Zurich na nyota huyo wa zamani wa Manchester United mebainisha kuwa ilibidi awaokoe nyota hao wa Barcelona. Ronaldo amesema wakati wakiwa juu ya jukwaa sio Neymar wala Messi ambaye anaweza kuzungumza kiingereza hivyo alibidi awe mkalimani wao na kutani kuwa alizungumza nao baadae na kuwaomba wamlipe.

No comments:

Post a Comment