Friday, January 29, 2016

DE BRUYNE NJE WIKI SITA.

KIUNGO mahiri wa Manchester City, Kevin De Bruyne anatarajiwa kukaa nje uwanja kwa kipindi cha wiki sita baada ya kupata majeruhi ya goti juzi. De Bruyne aliumia goti katika mchezo wa Kombe la Ligi ambao City walishinda kwa mabao 3-1 dhidi ya Everton na kutinga fainali ya michuano hiyo. Wakala wa mchezaji huyo, Patrick de Koster amesema amezungumza na mteja wake huyo na kumuahidi kuwa atarejea akiwa na nguvu zaidi. De Bruyne anatarajiwa kukosa mechi muhimu za timu yake ukiwemo ule wa fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya Liverpool utakaochezwa Februari 28 pamoja na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Dynamo Kiev.

No comments:

Post a Comment