Friday, January 29, 2016

GARY NEVILLE USO KWA USO NA BARCELONA KOMBE LA MFALME.

KLABU ya Valencia ambayo inanolewa na Muingereza Gary Neville jana ilifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mfalme baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Las Palmas. Valencia walitinga hatua hiyo kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wao wa mkondo wa kwanza. Valencia sasa watavaana na mabingwa watetezi wa michuano hiyo Barcelona katika mechi za mikondo miwili zitakazochezwa Februari 3 na 10. Nusu fainali nyingine ya michuano hiyo itaikutanisha Sevilla dhidi ya Celta Vigo. Mara ya mwisho Valencia kukutana na Barcelona ilikuwa Desemba mwaka jana ambapo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1, ikiwa ni siku tatu toka Neville ateuliwe kuwa kocha wa timu hiyo.

No comments:

Post a Comment