Thursday, January 28, 2016

TETESI ZA USAJILI ZILIZOJIRI HUKO MAJUU.

MSHAMBULIAJI nyota wa Bayern Munich, Roberto Lewandowski anadaiwa kuwa tayari kuondoka katika klabu hiyo majira ya kiangazi. Arsenal, Manchester United na Manchester City zote zimekuwa zikifuatilia nyendo za nyota huyo wa kimataifa wa Poland kwa karibu.
Chanzo: The Telegraph

KIUNGO wa West Ham United, Reece Oxford anatarajiwa kujiunga na Charlton Athletic kwa mkopo wa mpaka mwishoni mwa msimu baada ya kushindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza.
Chanzo: Various

KLABU ya Swansea City imetoa ofa ya paundi milioni saba kwa ajili ya mshambuliaji wa Crystal Palace Dwight Gayle ikiwa ni sehemu ya mikakati yao ya kuimarisha safu ya ushambuliaji.
Chanzo: The Guardian

PAMOJA na Alexandre Pato kukaribia kukamilisha uhamisho wake kwenda Chelsea, AC Milan wanadaiwa bado kuwa na nia ya kumrejesha mchezaji wao huyo wa zamani katika kipindi cha majira ya kiangazi. Milan wanataka kwanza kuona kiwango chake pindi atakapokuwa Stamford Bridge.
Chanzo: La Stampa

KLABU ya Watford inaripotiwa kukaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa Fiorentina Mario Suarez.
Chanzo: Marca

No comments:

Post a Comment