Thursday, January 28, 2016

BARCELONA, CELTA VIGO ZATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA MFALME.



MABINGWA watetezi wa Kombe la Mfalme, Barcelona wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuichapa Athletic Bilbao jana. Barcelona waliwachapa Bilbao mabao 3-1 ambayo yalifungwa na Luis Suarez, Gerrard Pique na Neymar na kuwafanya kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5-2 katika mechi za mikondo miwili walizokutana. Celta de Vigo nao walitinga hatua hiyo baada ya kuwaondosha vijana wa Diego Simeone, Atletico Madrid kwa kuwafunga mabao 3-2 timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana katika mchezo wao wa mkondo wa kwanza. Robo fainali nyingine inatarajiwa kuchezwa baadae leo ambapo Las Palmas watashuka dimbani kukwaana na Valencia huku Mirandes wao wakikabiliana na Sevilla.

No comments:

Post a Comment