Wednesday, January 27, 2016

TETESI ZA USAJILI ZILIZOJIRI HUKO MAJUU.

KLABU ya Watford inaripotiwa kuwa katika mazungumzo na Liverpool kuhusu uhamisho wa Jerome Sinclair. Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 19 mkataba wake unamalizika majira ya kiangazi na Liverpool wanataka paundi milioni tatu kama watamuuza kipidi hiki cha Januari.
Chanzo: Daily Mail

MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amekutana na wakala wa Granit Xhaka kuzungumzia uwezekano wa kumsajili kiungo huyo wa klabu ya Borussia Monchengladbach.
Chanzo: Sport Bild

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic amekuwa mchezaji anayelipwa zaidi Ufaransa toka mshahara wake uongezeke Januari hii mpaka kufikia kiasi cha euro milioni 1.5 kwa mwezi ukijumlisha na bakshishi.
Chanzo: Le Parisien

KLABU ya Leicester City imeweka dau la paundi ilioni 7.8 kwa ajili ya mshambuliaji wa Chelsea Loic Remy. Newcastle United na Swansea City nazo zinammezea mate nyota huyo.
Chanzo: L’Equipe

KLABU za Wolfsburg, Schalke na Bayer Leverkusen zinapigana vikumbo kumuwania winga wa Fenerbahce Caner Erkin mwenye umri wa miaka 27.
Chanzo: Fanatik

MENEJA wa Atletico Madrid, Diego Simeone anadaiwa kumwambia Fernando Torres kuwa hana mpango wa kumsajili moja kwa moja.

Chanzo: AS

MENEJA wa Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino anatajwa kuwepo katika orodha ya miongoni mwa makocha wanaowindwa na Chelsea kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Guus Hiddink mwishoni mwa msimu huu. Wengine katika orodha hiyo ni pamoja na Diego Simeone, Didier Deschamps na Jorge Sampaoli.
Chanzo: The Times

KLABU ya Chelsea inaripotiwa kumuweka Robin van Persie katika rada zake kama dili la kumnasa Alexandre Pato litashindikana.
Chanzo: Daily Express

No comments:

Post a Comment