Thursday, January 28, 2016

BARCELONA YAANZA KUMTOLEA MACHO DYBALA.

KLABU ya Barcelona wanatarajia kumpa kipaumbele mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala, katika usajili wao wa majira ya kiangazi. Mabingwa hao wa Hispania na Ulaya walikuwa wamemlenga Nolito wa Celta Vigo katika kipindi hiki cha usajili lakini sasa wamejitoa baada ya bodi ya klabu hiyo kujiridhisha kuwa usajili wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 hautakuwa na tija. Barcelona sasa wanadaiwa kuwa tayari wameanza mazungumzo ya mwanzo na Juventus wakati wakiendelea kumfuatilia kwa karibu Dybala ambaye amefunga mabao 12 na kusaidia mengine saba katika mechi 20 za Serie A alizocheza msimu huu. Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona, Robert Fernandez anaamini nyota huyo wa kimataifa wa Argentina atakuwa chaguo sahihi kwa klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment