MAKAMU wa rais wa Barcelona, Jordi Mestre haofii kumpoteza Neymar kwenda Real Madrid, kufuatia tetesi zilizozagaa zinazomhusisha mshambuliaji huyo kuhamia Santiago Bernabeu. Madrid wanadaiwa kuona kama Neymar mwenye umri wa miaka 23 kuwa mbadala wa Cristiano Ronaldo na taarifa zinadai kuwa tayari walishakutana naye katika sherehe za tuzo ya Ballon d’Or zilizofanyika jijini Zurich mapema mwezi huu. Neymar wenyewe tayari alishakanusha tarifa hizo za kukutana na wawakilishi wa Madrid lakini tetesi kuhusu mustakabali wake bado zimeendelea kuvuma kila pembe. Akihojiwa Mestre amesema haoni sababu yeyote ya Neymar kuondoka Barcelona kwani amekuwa akifurahia maisha ya hapo.
No comments:
Post a Comment