Thursday, January 21, 2016

TETESI ZA USAJILI ZILIZOJIRI HUKO MAJUU.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Brazil, Neymar na baba yake wameripotiwa kukutana na wawakilishi wa Real Madrid katika sherehe za utoaji tuzo za Ballon d’Or kujadili uhamisho baada ya mazungumzo ya mkataba mpya na Barcelona kusimama.
Chanzo: Onda Cero

WAKATI ikiripotiwa kuwa Chelsea wanakaribia kumsajili nyota wa kimataifa wa Brazil Alexandre Pato, hatua hiyo inaweza kushindikana baada ya Sporting Lisbon nao kutajwa kumuwania mchezaji huyo huku tayari wakiwa wameanza mazungumzo.
Chanzo: A Bola

KLABU ya Fulham itakuwa tayari kumuuza mshambuliaji wake Moussa Dembele kwa paundi milioni sita kwenda Tottenham Hoptspurs kipindi hiki cha Januari lakini watamuhitaji tena kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu.
Chanzo: Evening Standard

KIUNGO wa zamani za Bolton Wanderers, Newcastle United na West Ham United, Kevin Nolan anatarajiwa kutangazwa kama kocha-mchezaji wa klabu ya Leyton Orient ya Ufaransa kwa mkataba wa miaka miwili na nusu.
Chanzo: Sky Sports

KLABU ya Tottenham Hotspurs nao imeingia katika kinyang’anyiro cha kumuwania Alvaro Morata ili aweze kuja kuwa mbadala wa Harry Kane lakini wanakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Real Madrid, Arsenal na Manchester United ambazo nazo zimeonyesha nia ya kumtaka.
Chanzo: The London Evening Standard

NYOTA wa Chelsea Papy Djolobodji amefanyiwa vipimo vya afya kwa ajili ya uhamisho wake w mkopo kwenda Werder Bremen.
Chanzo: Daily Express


No comments:

Post a Comment