SHIRIKISHO la Soka la Ulaya-UEFA limedai kuwa bado wanaendelea kumlipa mshahara rais wake aliyefungiwa Michel Platini mpaka itakapoamuliwa vinginevyo. Taarifa hiyo ya UEFA imekuja baada ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA nalo kudai rais aliyefungiwa Sepp Blatter ataendelea kulipwa stahiki zake mpaka atakapochaguliwa rais mpya katika uchaguzi wa Februari 26. Platini na Blatter wote walisimamishwa kwa siku 90 na kamati ya maadili ya FIFA Octoba 8 mwaka jana na baadae kufungiwa kujishughulisha na masuala ya michezo kwa miaka nane mwezi uliopita. Adhabu ya wawili hao imekuja kufuatia malipo ya dola milioni mbili aliyopewa Platini kutoka kwa Blatter mwaka 2011 kufuatia kazi za soka zilizofanyika miaka nane iliyopita. Msemaji wa UEFA alithjibitisha Platini kuendelea kulipwa stahiki zake na ataendelea kulipwa mpaka utakavyoamuliwa vinginevyo.
No comments:
Post a Comment