Sunday, January 31, 2016

CHELSEA KUIVAA MAN CITY KATIKA ROUND YA TANO YA FA.

KLABU ya Chelsea imepangwa kucheza na Manchester City katika ratiba ya mzunguko wa tano ya michuano ya Kombe la FA iliyotolewa jana.Klabu ya League One ya Shrewsbury Town, timu pekee ya daraja la chini iliyobaki wenye wanatarajiwa kuwa wenyeji wa Manchester United huko New Meadow.Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Arsenal wao wataivaa Hull City ikiwa ni maruadio ya fainali ya mwaka 2014, wakati Crystal Palace wao watakuwa wageni wa Tottenham Hotspurs na Bournemouth wakiwa wenyeji wa Everton mechi mbili ambazo zitakutanisha timu zote za Ligi Kuu.Mechi zingine zitawakutanisha Watford dhidi ya Leeds United, Reading wakisubiri mshindi kati ya West Bromwich Albion na Peterborough wakati Blackburn Rovers nao wakisubiri mshindi katika mechi kati ya Liverpool na West Ham United.Mechi hizo za mzunguko wa tano zinatarajiwa kuchezwa wikiendi ya Februari 19 hadi 22 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment