Monday, February 1, 2016

HAKUNA USAJILI MWINGINE KWA ARSENAL LABDA ATOKEE MESSI - WENGER.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema ana uhakika wa asilimia 99 kuwa klabu hiyo haitafanya usajili katika dakika hizi za mwisho labda utokee uwezekano wa kumnasa Lionel Messi. Arsenal imemsajili Mohamed Elneny pekee katika kipindi hiki cha usajili wa Januari na kuifanya klabu hiyo kuwa kimya sana katika muda wote wa usajili. Wenger hategemei usajili wa dakika mwishoni kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo baadae saa sita usiku lakini amekiri kuwa itawezekana tu kama kuna mchezaji wa kipekee atakayetokea ghafla. Akihojiwa Wenger amesema kipindi chote cha usajili wa dirisha dogo kimekuwa kimya kuliko alivyotegemea na hilo limetokana na kukosekana kwa aina ya wachezaji aliowahitaji. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa maajabu yanaweza kutokea siku zote lakini ana uhakika wa asilimia 99 kuwa hakuna usajili mwingine utakaofanyika labda Messi atokee dakika za mwisho kwani hawezi kumkataa nyota huyo wa Barcelona.

No comments:

Post a Comment