Monday, February 1, 2016

AC MILAN YAACHANA NA DE JONG, AAMUA KUTIMKIA MERKANI.


KLABU ya AC Milan imethibitisha kusitisha mkataba wake na Nigel De Jong kufuatia kuwaniwa na klabu ya Los Angeles Galaxy ya Marekani. Kiungo huyo amecheza mechi tano pekee za Serie A msimu huu, pamoja na kuwa chaguo la kwanza katika kikosi cha Filippo Inzaghi msimu uliopita. Nyota huyo wa kimataifa wa Uholanzi amekuwa katika mzungumzo na Galaxy katika wiki za karibuni na Milan wamekubali kutengua mkataba wake. Taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo ilithibitisha mkataba wa De Jong kutenguliwa kwa maelewano na kumshukuru kiungo huyo kwa kujituma kwa bidii kwenye kipindi chote alichokuwepo San Siro.

No comments:

Post a Comment