Sunday, March 30, 2014

GUARDIOLA AIHOFIA MAN UNITED.

MENEJA wa klabu ya Bayern Munich, Pep Guardiola ameonyesha kutofurahishwa kiwango cha timu yake katika mchezo dhidi ya Hoffenheim jana na kutaka wachezaji wake kubadilika haraka kabla ya mchezo wao wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa UUlaya dhidi ya Manchester United utakaochezwa Jumanne ijayo katika Uwanja wa Old Trafford. Bayern ambao walitawadhwa mabingwa wa Bundesliga wiki iliyopita walionekana kama watashinda mechi yao ya 20 mfululizo katika Bungesliga baada ya kufunga mabao matatu mapema lakini Hoffenheim walijirudi na kuswazisha mabao yote hivyo timu hizo kwenda sare ya mabao 3-3. Akihojiwa Guardiola amesema Hoffenheim wanastahili pongezi kwa kucheza vyema katika mchezo huo na kuhakikisha wamepata alama. Kocha huyo aliendelea kusema jambo la muhimu ni kuyafanyia kazi mapungufu yao haraka kabla ya kukwaana na United wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment