Sunday, March 30, 2014

ANCELOTTI AWASHANGAA MASHABIKI WA MADRID KUMZOMEA RONALDO.

MENEJA wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti amewaponda mashabiki wa timu hiyo kwa kumzomea Cristiano Ronaldo katika ushindi wa mabao 5-0 waliopata kutoka kwa Rayo Vallecano jana usiku. Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno alifunga bao la kwanza mapema lakini alizomewa na baadhi ya mashabiki katika Uwanja wa Santiago Bernabeu kwa kushindwa kutoa pasi kwa wenzake sehemu zinakuwa ngumu hivyo kufanya mpira kupotea. Ancelotti amesema hajui kwanini mashabiki hao walikuwa wanamzomea Ronaldo kwasababu anadhani timu ilicheza vyema na kupata ushindi waliohitaji. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa ni jambo la kawaida kuzomewa muda mwingine kama hawachezi vyena lakini kwa jinsi hali ilivyokuwa jana hakuona umuhimu wa mashabiki hao kuzomea.

No comments:

Post a Comment