Sunday, March 30, 2014

KAKA AFURAHIA KUTIMIZA MECHI YA 300 MILAN.

NAHODHA wa klabu ya AC Milan, Kaka amefurahishwa na kiwango alichokionyesha katika ushindi wa mabao 3-0 waliopata dhidi ya Chievo jana akifikisha mechi yake ya 300 akiwa na klabu hiyo. Kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil alifunga mabao katika kila kipindi, baada ya Mario Balotelli kuipa timu hiyo ushindi wa mapema katika Uwanja wa San Siro na kuifanya timu hiyo kupata ushindi wake wa pili mfululizo. Kaka amesema usiku wa jana ulikuwa ni wa kukumbukwa kwake na amefurahishwa na jinsi alivyocheza sambamba na wachezaji wenzake. Pamoja na Kaka kufurahia ushindi huo mapema kabla ya mchezo huo Ofisa Mkuu wa Milan Adriano Galliani alibainisha kuwa nyota huyo anaweza kuondoka katika majira ya kiangazi.

No comments:

Post a Comment