Friday, March 28, 2014

RAMSEY KUIKOSA MAN CITY.

KIUNGO mahiri wa klabu ya Arsenal, Aaron Ramsey anatarajiwa kukosa mechi dhidi ya Manchester City mwishoni mwa wiki hii, baada ya kocha Arsene Wenger kuamua kutomharakisha nyota huyo wa kimataifa wa Wales kurejea kutoka katika majeruhi. Ramsey hatacheza mechi yoyote toka Desemba 26 mwaka jana wakati alipoumia kwenye mchezo dhidi ya West ham United ambao Arsenal walishinda kwa mabao 3-1. Wenger amebainisha kuwa wanatakiwa kuwa wavumilivu kwa nyota huyo ambaye amefunga mabao 13 katika mzunguko wa kwanza wa ligi aliocheza. Kocha huyo amesema Ramsey amekuwa akiendelea vizuri na tayari ameshaanza mazoezi na wenzake lakini inabidi kuvulia zaidi kwa wiki kadhaa kabla ya kumruhusu kurejea uwanjani rasmi. Wenger pia atawakosa nyota wake wengine kama Mesut Ozil na Jack Wilshere katika mchezo huo ambao City watasafiri kuifuata timu hiyo Emirates.

No comments:

Post a Comment