Friday, March 28, 2014

IBRAHIMOVIC YUKO KATIKA KIWANGO BORA MSIMU HUU - BLANC.

MENEJA wa klabu ya Paris Saint-Germain-PSG, Laurent Blanc anaamini kuwa Zlatan Ibrahimovic amekuwa katika msimu wake mzuri toka aanze kucheza soka. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Sweden amefunga mabao 40 katika mashindano yote akiwa na klabu yake hiyo na kuiwezesha kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea taji lao. Na kocha huyo ana uhakika nyota huyo wa zamani wa Barcelona na AC Milan anaweza kuendelea kucheza kwa kiwango cha juu mpaka mwishoni mwa msimu huu. Blanc amesema ana mategemeo Ibrahimovic ataendelea kufunga katika mechi muhimu zinazokuja na haoni kama hilo litamshinda. PSG inatarajiwa kusafiri kuifuata Nice Ijumaa katika mchezo wa ligi kabla ya kuikaribisha jijini Paris Chelsea kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza war obo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

No comments:

Post a Comment