Friday, March 28, 2014

MILANGO IKO WAZI KWA VALDES KAMA AKIAMUA KUBAKIA - BARTOMEU.

RAIS wa klabu ya Barcelona, Josep Maria Bartomeu amedai kuwa Victor Valdes bado hajaamua kubakia klabuni hapo katika majira ya kiangazi yanayokuja. Mkataba wa sasa wa Valdes unatarajiwa kumalizika Juni na golikipa huyo wa kimataifa wa Hispania ameweka wazi huko nyuma kuwa huu utakuwa msimu wake wa mwisho na Barcelona, huku Monaco na Manchester City zikihusishwa na kunyemelea saini yake. Hata hivyo, Bartomeu amesisitiza hana taarifa ya ofa yoyote ambayo Valdes amefikia na klabu nyingine na kudai kuwa milango bado iko wazi kama akiamua kubakia baada ya kupona majeraha ya goti aliyopata katika mchezo dhidi ya Celta Vigo. Bartomeu amesema tayari wameshamwambia Valdes kuwa klabu iko upande wake na kwasasa mawazo yake yako katika upasuaji atakaofanyiwa lakini anajua kuwa milango iko wazi kwa ajili yake.

No comments:

Post a Comment