Friday, March 28, 2014

MARTINEZ APANIA KUMWAGA MIHELA KIANGAZI.

MENEJA wa klabu ya Everton Roberto Martinez amekiri kuwa ana nia ya kutumia fedha kusajili kabla ya kuanza kwa msimu mwingine wa Ligi Kuu kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake. Martinez alithibitisha hilo jana kuwa atatumia fedha katika kipindi cha usajili kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2014-2015 baada ya kujiweka katika nafasi nzuri msimu huu toka achukue mikoba ya kuinoa klabu hiyo Juni mwaka jana. Kocha huyo alimuuza Maroune Fellaini, Nikica Jelavic na Victor Anichebe wakati pia alimtoa kwa mkopo John Heitinga hivyo kuikusanyia klabu paundi milioni 40 na kupunguza mzigo wa mshahara. Martinez alibainisha kuwa hakutumia fedha zozote katika kipindi cha Januari hivyo wakati huo ndio utakuwa muafaka kutumia fedha hizo na nyingune atakazopewa ili kuimarisha kikosi hicho.

No comments:

Post a Comment