MENEJA wa klabu ya Borussia Dortmund, Jurgen Klopp amehuzunishwa na kitendo cha Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA kutowashirikisha makocha au wachezaji juu ya michuano mipya ya Ligi ya Mataifa. Michuano hiyo ambayo itashuhudia timu za Ulaya zikigawanywa katika makundi manne, imeanzishwa kwa madhumuni ya kuchukua nafasi ya kalenda ya mechi za kirafiki na kuleta ushindani zaidi. Hata hivyo, Klopp anafikiri mechi zitakazochezwa katika michuano hiyo zitahitaji nguvu zaidi za wachezaji. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 46 amesema anafikiri uamuzi huo ungekuwa tofauti kama viongozi waliotoa uamuzi huo wangekuwa pia wanatakiwa kucheza mechi hizo. Klopp amesema ingekuwa vyema zaidi kama UEFA wangewashirikisha makocha na wachezaji kwa ushauri juu ya uamuzi huo.
No comments:
Post a Comment