Tuesday, March 25, 2014

MMILIKI WA RED BULL ATISHIA KUJITOA MASHINDANO YA LANGALANGA.

MMILIKI wa Red Bull, Dietrich Mateschitz amesema kampuni yake inaweza kujitoa katika mashindano ya langalanga kama hatafurahishwa na jinsi mchezo huo unavyoendeshwa. Kauli yake hiyo imekuja kufuatia dereva wake wa Red Bull Daniel Ricciardo kuenguliwa katika mashindano ya Grand Prix ya Australia na sheria mpya zilizowekwa. Tajiri huyo amesema kuna kiwango cha mambo ambayo watayakubali lakini akiona kama masuala ya siasa yanazidi katika mchezo huo hawatakuwa na budi bali kujitoa. Red Bull imekata rufani dhidi Ricciardo kwa kutolewa katika mashindano hayo ya mwanzoni mwa msimu yaliyofanyika jijini Melbourne kwa kutumia mafuta mengi kuliko ilivyostahili katika sheria mpya na rufani hiyo inatarajiwa kusikilizwa April 14 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment