Monday, March 31, 2014

FAINALI YA KOMBE LA DUNIA 2010 ILIKUWA NGUMU - WEBB.

MWAMUZI Howard Webb wa Uingereza amekiri kuwa kuna maamuzi moja au mawili ambayo anatamani angeamua tofauti katika mchezo wa fainali ya Kombe la dunia mwaka 2010. Katika fainali hiyo ambayo ilishuhudia Hispania iliitandika Uholanzi kwa bao 1-0 baada ya muda wa nyongeza bao ambalo lilifungwa na Andres Iniesta, Webb alitoa kadi za njano 14 katika dakika 120 zilizochezwa. John Heitinga alitolewa nje kwa kadi nyekundu muda mfupi baada ya Hispania kufunga bao la kuongoza huku faulo ya Nigel de Jong kumrukia teke la karate Xabi Alonso ikilalamikiwa ilitakiwa kuwa kadi nyekundu lakini mchezaji huyo hakutolewa kwa kupewa kadi ya njano pekee. Mwamuzi huyo wa Ligi Kuu anatarajiwa kurejea tena katika michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Brazil kipindi cha kiangazi, ameelezea mapungufu machache aliyofanya katika michuano hiyo iliyopita. Webb aliyekuwa mwamuzi katika mchezo huo amesema pamoja na kwamba mchezo ulikuwa mgumu ni maamuzi machache kama angepata nafasi angeyabadili lakini kwa muda ule unatakiwa kufanya uamuzi kutokana na maelezo uliyonayo na nafasi uliyopo.

No comments:

Post a Comment