Monday, March 31, 2014

KANKAVA APONGEZWA KWA KUOKOA MAISHA YA MCHEZAJI MWENZAKE.

KIUNGO wa klabu ya Dnipro, Jaba Kankava amepongezwa kwa kuokoa maisha ya nahodha wa Dynamo Kiev Oleg Gusev katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Ukraine uliochezwa jana. Gusev alimeza ulimi wake baada ya kugongwa na goti kwa bahati mbaya na kipa wa Dnipro Denis Boyko katika dakika ya 22 ya mchezo na Kankava alikimbia haraka eneo hilo na kuhakikisha anampatia huduma ya kwanza Gusev kabla ya madaktari hawajafika. Gusev alizinduka akiwa katika machela kabla ya kupelekwa katika kliniki ya Boris iliyopo Dnipropettrovsk huku daktari mkuu Mikhail Radutskyy akipongeza uwezo wa haraka wa kufikiri wa Kankava kwa kuepusha janga kubwa ambalo lingeweza kutokea. Daktari amesema ingawa Gusev kwasasa anaendelea vyema lakini ujasiri alioonyesha Kankava ndio uliookoa maisha ya nahodha huyo na kama angechelewa kupata huduma hiyo pengine angeweza kupoteza maisha. Katika mchezo huo Dnipro walishinda kwa mabao 2-0 na kukwea mpaka nafasi ya pili katika msimamo wa ligi wakiwa nyuma ya vinara Shakhtar Donetsk.

No comments:

Post a Comment