Monday, March 31, 2014

DJOKOVIC ASHINDA TAJI LA SONY OPEN KWA KUMTANDIKA NADAL.

NYOTA wa tenisi Novak Djokovic amefanikiwa kushinda taji la michuano ya wazi ya Sony kwa kumtandika Rafael Nadal katika mchezo wa fainali uliofanyika jijini Miami. Djokivic raia wa Serbia mwenye umri wa miaka 26 alishinda mchezo huo kwa 6-3 6-3 ushindi uliompa taji la nne la michuano hiyo akimzidi Peter Sampras na kuwa nyuma ya nguli mwingine Andre Agassi aliyenyakuwa taji la michuano hiyo mara sita. Baada ya kushindwa kufanya vizuri katika msimu wa viwanja vigumu, Nadal mwenye umri wa miaka 27 anategemea kufanya vizuri wakati ziara ikienda Ulaya kwenye viwanja vya udongo ambapo alifanya vyema kwenye viwanja hivyo msimu uliopita. Katika mchezo huo Djokovic hakuwa na mwalimu wake Boris Becker ambaye anauguza majeraha ya paja baada ya kufanyiwa upasuaji.

No comments:

Post a Comment