Monday, March 31, 2014

PELLEGRINI AMPASHA CHADOMO MOURINHO.

MENEJA wa klabu ya Manchester City, Manuel Pellegrini amempasha meneja wa Chelsea Jose Mourinho kuwa kocha yoyote mwenye ujuzi huwa hachezi na akili za watu. Kauli hiyo ya Pellegrini imekuja muda mfupi baada ya Mourinho kudai kuwa timu yake haiku katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu pamoja na ukweli kuwa walioongoza ligi hiyo kwa wiki kadhaa. Mourinho alienda mbali zaidi Jumamosi akidai kuwa ni suala lisilowezekana kwa timu yake kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza toka mwaka 2010 kufuatia kipigo cha kushtusha kutoka kwa Crystal Palace. Lakini Pellegrini amesisitiza kuwa mbinu anazotumia Mourinho haziwezi kumsaidia kwasababu hadhani kama kuna meneja yoyote anayetilia maanani mawazo yake. Pellegrini amesema huwa hajishughulishi kumjibu kwasababu hamwelewi anachosema.

No comments:

Post a Comment