MABINGWA watetezi Al Ahly ya Misri wameenguliwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika lakini wenzao Zamalek wamefanikiwa kusonga mbele. Al Ahly yenye maskani yake jijini Cairo walipoteza mchezo wao wa mkondo wa pili hatua ya timu 16 bora kwa kufungwa mabao 2-3 dhidi ya Al Ahli Benghazi ya Libya. Kwa ushindi huo Al Ahly ambao waliing’oa Yanga katika michuano hiyo nao wameng’olewa kwa jumla ya 4-2 na kuifanya Al Ahli Benghazi kutinga hatua muhimu ya makundi. Timu zote zilizoshindwa kusonga mbele baada ya mechi zao za mkondo wa pili zinaangukia katika michuano ya Kombe la Shirikisho ambapo watatakiwa kucheza hatua ya mtoano kabla ya kuingia katika hatua ya makundi katika michuano hiyo. Katika mechi zingine zilizochezwa jana za michuano hiyo Esperance ya Tunisia nao walifanikiwa kusonga mbele kwajumla ya mabao 4-1 baada ya kuifunga Real Bamako ya Mali kwa mabao 3-0. Wengine ni Zamalek ambao nao walisonga mbele kwa jumla ya mabao 5-0 katika mechi walizokutana na Nkana ya Zambia huku Entente Setif nao wakisonga mbele baada ya kiondosha Coton Sport ya Cameroon kwa jumla ya mabao 2-0.
No comments:
Post a Comment