Monday, March 31, 2014

RODGERS ATAMBA LIVERPOOL KUENDELEA KUJITANUA KILELENI.

MENEJA wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers ana uhakika wa timu yake kukabiliana na changamoto za ushindani wa ubingwa baada ya kurejea kileleni mwa msimo wa Ligi Kuu nchini Uingereza. Liverpool jana usiku waliichabanga Tottenham Hotspurs kwa mabao 4-0 na wanaweza kutawadhwa mabingwa wapya wa ligi hiyo kama wakifanikiwa kushinda mechi zao sita zilizobakia. Rodgers amesema bado alama nyingi zinahitajika na pia itafika mahali mahali kila timu itapoteza alama kabla ya kumalikia kwa msimu hivyo hana hofu yoyote kwasababu ana uhakika na wanavyocheza. Mara ya mwisho Liverpool kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ilikuwa ni Desemba 26 mwaka jana na sasa wamerejea tena baada ya ushindi huo mnono dhidi ya timu ngumu ya Spurs. Liverpool wakiwa wamebakiwa na mechi zingine ngumu mbili dhidi ya mahasimu wao katika kinyang’anyiro cha ligi hiyo City na Chelsea, wanategemea kunyakuwa taji hilo kwa mara ya kwanza toka walipofanya hivyo msimu wa 1989-1990.

No comments:

Post a Comment