Wednesday, March 26, 2014

KEWELL AAMUA KUTUNDIKA DARUGA.

WINGA wa zamani wa klabu ya Leeds United na Liverpool, Harry Kewell ametangaza rasmi kutundika daruga zake baada ya kucheza soka kwa karibu miongo miwili. Nyota huyo wa kimataifa wa Australia mwenye umri wa miaka 35 alirejea nyumbani kwao na kujiunga na klabu ya Melbourne Heart hatua ambayo ilichukuliwa kama kutafuta nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia baadae mwaka huu nchini Brazil. Hata hivyo mkongwe huyo alishindwa kuwa fiti kwa kukosa mechi tisa katika msimu huu kutokana na kuandamwa na majeruhi ya mara kwa mara. Kewell amesema baada ya kufikiria sana na kupata ushauri wa familia na marafiki ameona ni bora akatundika daruga ingawa bado angetamani kuendelea kucheza. Nyota huyo amesema pamoja na akili kumtaka kuendelea kucheza lakini mwili unaonekana kushindwa kumpa ushirikiano ndio maana ameamua kupumzika.

No comments:

Post a Comment