Wednesday, March 26, 2014

MOYES AKUBALI LAWAMA ZOTE.

MENEJA wa klabu ya Manchester United, David Moyes amekubali kubeba lawama zote kwa kuporomoka kwa klabu hiyo msimu huu baada ya kipigo walichopata kutoka kwa mahasimu wao Manchester City katika Uwanja wa Old Trafford. Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu kwasasa wako nafasi ya saba kwa tofauti ya alama 18 na vinara Chelsea baada ya timu hiyo kufungwa kwa mara ya sita kwenye uwanja wake nyumbani msimu huu. Moyes amesema yeye huwa anachagua kikosi cha kucheza hivyo anakubali lawama zote, huku akidai kuwa alijua utakuwa mwaka mgumu lakini alitegemea wataleta ushindani. Kipigo hicho kinamaanisha kuwa United wamepoteza mechi nyingi zaidi nyumbani kuliko ukijumlisha misimu mitatu iliyopita. Katika mechi tisa dhidi ya timu kubwa za Ligi Kuu wamefanikiwa kushinda mechi moja dhidi ya Arsenal Novemba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment