Monday, March 31, 2014

NAPOLI KUMPA REINA MKATABA WA KUDUMU.

RAIS wa klabu ya Napoli, Aurelio De Laurentiis amethibitisha kuwa wanaangalia uwezekano wa kumbakisha golikipa Pepe Reina zaidi baada ya kumalizika kwa msimu huu. Reina mwenye umri wa miaka 31 yuko Napoli kwa mkopo wa msimu mmoja kutoka klabu ya Liverpool na amekuwa akicheza vyema katika kipindi alichokuwepo katika Uwanja wa San Paolo chini ya kocha Rafa Banitez. Kufuatia ushindi mnono wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya Juventus jana ambao umefufua matumani yao ya kuwashika Roma waliopo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Serie A, De Laurentiis amebainisha kuwa wanaweza kumpa mkataba wa kudumu golikipa huyo wa kimataifa wa Hispania. Rais huyo amesema ameshazungumza na Reina, kama watamaliza ligi wakiwa katika nafasi ya pili atawazadia wote lakini pia anataka golikipa huyo abakie.

No comments:

Post a Comment