Saturday, March 22, 2014

MICHUANO YA SONY OPEN YAZIDI KUNOGA.

BINGWA mtetezi Andy Murray amefanikiwa kumfunga Matthew Ebden wa Australia na kutinga mzunguko wa tatu wa michuano ya wazi ya Sony inayofanyika jijini Miami, Marekani. Haikuwa kazi rahisi kwa Murray kutinga hatua hiyo kwani alipoteza seti ya kwanza kabla ya kuzinduka na kufanikiwa kumshinda Abden kwa 3-6 6-0 6-1. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Murray amesema kitendo cha kumkosa kocha wake wa siku nyingi ambaye alimtimua wiki iliyopita, imekuwa ngumu lakini anakiwa kusahau hayo na kuhakikisha anacheza kwa kiango bora zaidi. Murray ambaye alimfunga David Ferrer katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo iliyochezwa mwaka jana, sasa ataungana na Novak Djokovic na bingwa mara mbili wa michuano hiyo Roger Federer katika hatua inayofuata.

No comments:

Post a Comment