Tuesday, March 25, 2014

MJI WA PORTO ALEGRI HATARINI KUSHINDWA KUANDAA KOMBE LA DUNIA.

MEYA wa mji wa Porto Alegre uliopo kusini mwa Brazil amesema mji wake unaweza kujitoa kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia Juni mwaka huu kama sheria muhimu hazitapitishwa wiki hii. Jose Fortunati aliviambia vyombo vya habari nchini humo kuwa hakuna mpango mwingine wa kutafuta fedha nyingine nyingi zinazohitajika kwa ajili ya kukamilisha maandalizi yake. Michuano ya Kombe la Dunia inatarajiwa kuanza Juni 12 lakini kuna baadhi ya miji bado haijamaliza ujenzi wake. Uwanja wa Beira Rio uliopo Porto Alegre uko katika hatua za mwisho lakini bado unahitaji nyumba za muda mfupi kwa ajili ya vyombo vya habari, wadhamini na mambo mengine ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA.

No comments:

Post a Comment