Tuesday, March 25, 2014

UJERUMANI YAKATAA MFUMO WA TEKNOLOGIA YA KOMPYUTA KATIKA MSTARI WA GOLI.

Mpira ukiingia pembeni ya nyavu na mwmauzi kukubali kuwa bao katika mchezo kati ya Bayer Leverkusen na Hoffenheim
LIGI ya Ujerumani haitatumia mfumo wa teknologia ya kompyuta katika mstari wa goli kufuatia kura zilizopigwa na timu zinazoshiriki ligi za juu. Katika kura hizo kulikuwa kunahitajika theluthi mbili ya kura kati ya timu zinazoshiriki Bundesliga na zile za Ligi Daraja la Kwanza lakini ni timu tatu pekee kati ya 18 za daraja hilo zilipiga kura ya kukubali mfumo huo. Ligi Kuu nchini Uingereza imeshaanza kutumia mfumo huo msimu huu na utatumika pia katika michuano ya Kombe la Dunia katika kipindi cha majira ya kiangazi nchini Brazil. Rais wa Ligi za Soka nchini Ujerumani Reinhard Rauball amesema suala hilo wameshaliondoa mezani kwasasa kutokana na kura kutofikia. Suala la matumizi ya mfumo huo lilizua mjadala mkubwa Octoba mwaka jana wakati mwamuzi Stefan Kiessling alipowapa bao Bayer Leverkusen katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Hoffenheim ingawa mpira uliingia wavuni kupitia katika tundu lililokuwa pembezoni mwa neti. Hoffenheim walikata rufani mchezo huo urudiwe lakini ikatupiliwa mbali.

No comments:

Post a Comment