Tuesday, March 25, 2014

RANIERI AMSAMEHE ABIDAL BAADA YA KUOMBA RADHI.

MENEJA wa klabu ya Monaco, Claudio Ranieri amemrejesha Erick Abidal katika kikosi chake baada ya beki huyo kuomba radhi kwa kuondoka katika benchi la wachezaji wa akiba bila kuaga mwishoni mwa wiki iliyopita. Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa, aliondoka katika Uwanja wa Louis II kabla ya mchezo wa ligi kati ya Monaco na Lille ikiripotiwa kuwa alifanya hivyo baada ya kugundua hatakuwepo katika kikosi cha kwanza kwenye mchezo huo. Hata hivyo, Ranieri amethibitisha kuwa Abidal atakuwepo katika kikosi chake katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Ufaransa baada ya kuomba kwa kitendo hicho. Ranieri amesema hana tatizo na Abidal tena kwasababu kulifanyika mkutano na makamu wa rais wa klabu hiyo Vadim Vasilyev na ameomba radhi. Abidal mwenyewe aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akiwaomba radhi mashabiki na wachezaji wenzake kwa kitendo chake hicho huku akidai mambo yameshakwisha na kila kitu kiko sawa.

No comments:

Post a Comment