Thursday, March 27, 2014

BARCELONA YAMNASA MESSI MWINGINE KUTOKA DINAMO ZAGREB.

KLABU ya Barcelona imethibitisha kumsajili mchezaji nyota chipukizi Alen Halilovic kutoka klabu ya Dinamo Zagreb. Nyota huyo anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji amekuwa akiwindwa na vilabu mbalimbali barani Ulaya ikiwemo Manchester City, lakini ni Barcelona waliofanikiwa baada ya kutuma ujumbe wao nchini Croatia kumaliza dili hilo. Kinda huyo mwenye umri wa miaka 17 ambaye anatokana na matunda ya shule ya vipaji ya Dinamo amesaini mkataba wa miaka mitano kwa ada ya euro milioni 2.2. Akihojiwa Halilovic ambaye anafananishwa na Messi mdogo amesema ni ngumu kupata maneno ya kuzungumza jinsi anavyojisikia lakini anaishukuru sana Dinamo ambao atawapenda siku zote kwa kumfikisha hapo alipo sasa. Pia kinda huyo aliwashukuru makocha katika shule ya Dinamo waliomfundisha mpaka kufikia sambamba na mashabiki ambao mara zote wamekuwa nyuma yake.

No comments:

Post a Comment